1.kokwa la Embe




Unga wa Mbegu za maembe


Kutumia mbegu kubwa za maembe ni namna nyingine rahisi ya kutibu bawasiri hasa ya ndani inayotoa damu.


Tumia kama ifuatavyo:


Chukua mbegu za maembe (kokwa) toka katika maembe yaliyoiva, zianike juani kwa siku kadhaa na zikikauka kabisa zitwange au peleka mashineni upate unga wake na uuhifadhi unga ndani ya chupa isiyopitisha hewa.


Kisha changanya gramu 2 za unga huu na kiasi kidogo cha asali na ulambe yote. Fanya hivi kutwa mara 2 kwa majuma kadhaa.


Kwa faida ya ziada ni kuwa Unga huu wa mbegu za maembe hutumika pia kukaza uke uliolegea au ulioongezeka sana ukuwa.

2.

Jitibu kwa mkaratusi.


Mkaratusi ni moja ya mimea tiba ambayo hutumika zaidi duniani kutokana na nguvu yake ya kipekee ya kupambana na magonjwa kama vile pumu, kisukari, maumivu ya misuli na maungio ya mifupa na magonjwa ya ngozi.


Nguvu ya kutibu ya mkaratusi inatokana na dutu/kemikali zifuatazo ambazo hupatikana katika mmea huo;


👉Meliacins

👉Liminoids.

👉Tripterpenoid bitters

👉sterols

👉Tannis.

👉Flavanoids.


Kemikali hizi zina uwezo wa kuua na kuangamiza aina mbalimbali ya vimelea vya magonjwa vikiwemo vile vya magonjwa ya ngozi kama fangasi, pia kemikali hizi huweza kuiga na kufanya kazi zifanywazo na homoni mabalimbali za mwili kama vile insulini jambo linalofanya mkaratusi kuwa moja ya tiba kubwa ya asili ya kisukari.


Baadhi ya magonjwa ambayo hutibiwa na mkaratusi ni pamoja na;


Kutibu kisukari hasa kile kinachosababishwa na seli za ini kutengeneza kiasi kidogo cha homoni ya insulini au seli kushindwa za mwili kushindwa kutambua uwepo wa homoni za insulini.


Utafiti unaonesha matumizi ya majani na mafuta yatokanayo na mkaratusi ya uwezo wa kurekebisha kiwango cha sukari mwilini.


Majani ya mkaratusi yakichemshwa na kutumika kwa kunywa huweza kusaidia kutibu malaria, vidonda vya tumbo na magonjwa ya minyoo.na pia huweza kutumika kwa kupaka kwa mtu aliye na matatizo ya ngozi.


Juisi ya mkaratusi ambayo hutokana na majani hutumika kutibu watu wenye matatizo ya macho(watu wenye matatizo ya kuona usiku) kwa kupaka machoni.Matawi yaliyoshika majani ya mkaratusi yakitumika kama mswaki husaidia kujikinga na magonjwa ya kinywa kama kutoka damu katika uvizi.


Mafuta yatokanayo na mkaratusi hutumika kama chakula bora cha nywele na kuzisaidia nywele kukua vyema na pia mafuta haya yana uwezo wa kuua na kuangamiza vimelea vya magonjwa aina mbalimbali kama fukusi, bakteria na minyoo.


Jinsi ya kuandaa mkaratusi ili uweze kutumika kama mmea tiba.


Majani ya mkaratusi huchanganywa na maji na kuchemshwa kidogo na kuchujwa, maji yanayopatikana hutumiwa kwa kupaka katika ngozi kwa ajili ya kutibu magonjwa ya ngozi.


Matawi madogo hasa yaliyoshikilia majani hutumika kama mswaki na husaidia kuweka knywa katika hali nadhifu na kuulinda dhidi ya magonjwa ya kinywa.


Mbegu za mkaratusi zina mafuta, mafuta hayo yakivunwa husaidia kupambana na visubi aina ya chawa na mba za kichwani.


mafuta hayo hupakwa mara moja kwa siku kwa muda usiopungua majuma mawili.


ZINGATIA,


Maumizi yasiyo sahihi ya mkaratusi yanamadhara katika mfumo wa uzazi kwa vile hupunguza uwezo wa urutubishwaji wa mbegu za uzazi za mwanamke na mwanaume, na pia hairuhusiwi kwa mama anyenyonyesha kutumia mkaratusi kama tiba.


Kwa watoto mkaratusi utumike kwa kupaka tu na si kunywa.



3,Matumizi ya mbaazi kama dawa



Mbaazi ni zao la chakula ambalo linalimwa sehemu nyingi sana hapa nchini, zao hili pia linaweza kutumika kama dawa kwa kutumia majani, mizizi na maua


MAANDALIZI


Chukua majani, maua au mizizi kiasi cha nusu kilo (ni vizuri kama utachanganya vyote) pondaponda na uloweke kwenye maji safi kiasi cha lita 2 kwa muda wa masaa 24.


Chuja na uweke dawa hii mbali na jua/joto, ni vizuri kama utaweka kwenye friji, kunywa kikombe kimoja kutwa mara 3 kwa siku 3


Inatibu 


Dawa hii inaweza kutibu magonjwa yafuatayo


1-Inauwezo mkubwa wa kushusha homa


2-Husaidia kuponesha vidonda.


3-Husaidia kurekebisha mzunguko wa hedhi kwa wanawake.


4-Husaidia kupunguza uvimbe


5-Huponyesha kifua na kukohoa.


6-Husafisha kibofu/njia ya mkojo.


7- Huongeza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbali mbali.


Kwa Tiba zilizoandaliwa kitaalamu

uisi ya kitunguu maji husaidia kukuza nywele sababu inayo sulfur nyingi ya kutosha ambayo husaidia kuimarisha mzunguko wa damu kwenda kwenye vinyweleo vya nywele, huvifufua upya vinyweleo vya nywele na kupunguza uvimbe.


4, kitunguu maji


Kitunguu maji huua bakteria wabaya kitendo kinachosadia kuua vimelea na wadudu  wa magonjwa kwenye ngozi ya kichwa vitu ambavyo huweza kupelekea kupotea kwa nywele (upara).


Utafiti unaonyesha juisi ya kitunguu kuwa na uwezo mkubwa kutibu tatizo la kupotea kwa nywele kwa mjibu wa utafiti uliofanywa na Jarida la Dermatology mwaka 2002 huku wakitoa majibu ya zaidi ya asilimia 74 ya washiriki wa utafiti huo kupata kurejeshewa nywele zao zilizokuwa zimeanza kupotea.


Chukua juisi ya kitunguu maji kimoja na uipake moja kwa moja sehemu ambayo nywele zimeanza kupotea na uache kwa dakika 30 kisha jioshe baadaye na shampoo


Au changanya pamoja vijiko vikubwa vitatu vya chakula vya juisi ya kitunguu maji na vijiko vikubwa vingine viwili vya jeli ya aloe vera. Unaweza pia kuongeza kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya zeituni na upake mchanganyiko huo kichwani sehemu ambayo nywele zimeanza kupotea. Acha kwa dakika 30 ujisafishe na shampoo baadaye.


Rudia zoezi hili mara 2 mpaka 3 kwa wiki kwa wiki kadhaa.