Ticker

6/recent/ticker-posts

Faida za ulaji wa mayai

 




FAIDA ZA ULAJI WA MAYAI MWILINI


1️⃣MAYAI HUMSAIDIA MTUMIAJI KUBORESHA UFANISI KIUTENDAJI:


✍🏻Humsaidia mtumiaji kuhisi mwenye shibe kwa kipindi kirefu. Hii inatokana na ukweli kwamba yai moja kubwa lina uwezo wa kukupatia protini yenye ubora mkubwa na virutubisho mbalimbal muhimu vinavyohitajika mwilini isipokuwa vitamin C. 


✍🏻Ndiyo maana inashauriwa kujumuisha matunda au juisi ya machungwa yai, na mkate uliotayarishwa kwa unga wa ata hukupatia kifungua kinywa (breakfast) kilichokamilika humwezesha mtumiaji kuwa katika hali nzuri kiafya na hivyo kuweza kukabiliana vilivyo na changamoto mbalimbali za maisha.


 2️⃣HUONDOSHA MATATIZO MWILINI


✍🏻Watu wengi wenye upungufu wa madini ya chuma mwilini huhisi dalili mbalimbali za uchovu, kuumwa vichwa na kuwashwa ngozi. Madini haya ndiyo yanayobeba hewa ya oksijeni kwenye damu na hufanya kazi muhimu katika kuimarisha kinga za mwili na ufanisi wa nishati na kazi zingine mwilini. 


✍🏻Madini ya chuma yanayopatikana kwenye kiini cha yai kwenye mfumo ambao huwa tayari kufyonzwa na kutumika mwilini kuliko aina ya chuma ambazo hupatikana kwenye virutubisho vingine vya vyakula.


3️⃣HUBORESHA UTOSHELEZAJI WA VIRUTUBISHO KWENYE LISHE:


✍🏻Idadi ya virutubisho vilivyomo kwenye mayai huyafanya kuwa na mchango muhimu kwenye lishe yenye virutubisho. Utafiti uliofanywa baina ya lishe inayotumiwa na walaji mayai na wasiotumia mayai zimebaini kwamba lishe za walaji wasiotumia mayai kuwa na mapungufu

makubwa ya ya vitamin A, E na B12. 


✍🏻Mayai huchangia kiasi cha asilimia 10-20 ya madini ya folate na kiasi cha asilimia 20-30 za vitamin A, E na B12 kwa watumiaji wake.


4️⃣MAYAI HAYAONGEZI LEHEMU KWENYE DAMU:


✍🏻Mnamo mwaka 1990 mayai yalitangwaza vibaya kutokana na kiwango cha lehemu ambacho ni miligramu 210 kwa kila kiini cha yai. Lakini hata hivyo tafiti nyingi zimethibitisha kutokuwepo mahusiano yeyote ya ulaji mayai na magonjwa ya moyo na kuweka mambo kwenye mtazamo wa wazi ni vema kufahamu kwamba vyakula vyenye kiasi kikubwa cha mafuta yatokanayo na wanyama (saturated fatty acids) ndivyo vyenye athari kubwa kiasi cha kusababisha maradhi ya moyo. 


✍🏻Hivyo ni vema tukatambua kwamba mayai ni chanzo nafuu cha protini, ambacho pia ni chepesi kusagwa na kusharabiwa mwilini na kuweza kutumika kwa namna mbalimbali.


5️⃣MAYAI HUWEZA KUMSAIDIA MTUMIAJI KUPUNGUZA UZITO WAKE:


✍🏻Mayai yakiliwa kama toast (mkate uliopakwa mayai na kuokwa) una uwezo wa kumpa uhakika wa usalama mlaji kwa asilimia 50 kuliko utumiaji wa mara kwa mara wa vifungua kinywa vya nafaka (cereals). Tafiti mbalimbali zimethibitisha kwamba kuanza siku kwa kifungua kinywa chenye yai huwaongezea uhakika wa afya zao watu walio na uzito uliopitiliza na huweza kuwasaidia kupunguza sehemu ya uzito wao. 


✍🏻Kwa mfano tafi ti moja ambapo kifungua kinywa cha mkate uliookwa na nyama na kupakwa krimu ya siagi na maziwa mgando ililinganishwa na kifungua kinywa kingine cha mkate uliookwa kwa maya mawili (toast) na jamu ya matunda. 


✍🏻Vifungua kinywa vyote vikiwa na virutubisho vinavyolingana. Tafiti hii ilibaini kwamba kundi la walaji lililotumia aina ya pili ya kifungua kinywa lilidumu na shibe kwa muda mrefu na hivyo kula kiasi kidogo cha chakula cha mchana (lunch) na hivyo kuthibitisha zaidi kuwa mayai yana uwezo mkubwa wa kupunguza uzito iwapo yatatumiwa. Hii ni kwa kumpunguzia mlaji kula mara kwa mara na hivyo kupunguza uzito.


6️⃣HUSAIDIA KUBORESHA AFYA YA UBONGO:


✍🏻Kirutubisho kijulikanacho kitaalamu kama choline husaidia kuboresha ubongo wa kiinitete (foetus) na watoto wadogo na hata kumbukumbu kwa wazee. 


✍🏻Mayai ni lishe yenye chanzo kizuri cha kirutubisho hiki cha choline na yai moja kwa siku humpatia mama mjazito asilimia 28 ya kirutubisho hiki. Kirutubisho cha choline ni muhimu sana hasa wakati wa ujauzito na unyonyeshaji pale ambapo akiba ya mwilini inapokuwa imepungua. 


✍🏻Huu ni wakati muhimu wa kukua kwa ubongo kiinitete na uboreshwaji wa kumbukumbu ya muda wote wa maisha.


7️⃣HUPUNGUZA UWEZEKANO WA KUPATA MAGONJWA YA MACHO NA KUBORESHA UWEZO WA KUONA:


NOTE:.. kupata taarifa za afya Kila siku shuka chini utaona sehemu ya kusubscribe weka email yako afu gusa subscribe utapata post Kila siku

  Iko hivi::



Post a Comment

0 Comments