SABABU ZA TATIZO LA MBEGU CHACHE ZA KIUME(LOW SPERM COUNT)
Watu wengi hudhani kama mwanamke hapati ujauzito basi tatizo na lawama zote zitakuwa ni upande wa mwanamke, lakini hilo si lazima mara zote liwe hivyo. Kuna uwezekano mkubwa kuwa tatizo la kutopata mtoto katika familia likawa linatokana na ugumba upande wa mwanaume.
Mwanaume kuzalisha mbegu chache kuliko kawaida ni mojawapo ya sababu kubwa za ugumba kwa wanaume.
MBEGU CHACHE NI KIASI GANI?
Shahawa kawaida ni mchanganyiko wa maji maji (ute) unaotengenezwa na tezi dume na mbegu za kiume (manii). Mtu anakua na tatizo la mbegu chache pale katika kila Millilita moja ya shahawa zake kunakua na mbegu (manii) chini ya millioni 15. Kwa kawaida mwanaume anazalisha zaidi ya manii millioni 20 katika kila millilita moja ya shahawa anazomwaga.
Kitaalamu tatizo hili linaitwa OLIGOSPERMIA (ol-ih-go-spur-me-uh), na kutokuwa na mbegu za kiume kabisa kwenye shahawa inajulikana kama AZOOSPERMIA
DALILI
Dalili kuu ya tatizo hili ni kushindwa kutungisha mimba/kupata mtoto.Zinaweza kuwepo dalili nyingine kulingana na chanzo cha tatizo hili mfano mirija ya manii kuziba,matatizo kwenye korodani na matatizo kwenye mfumo wa hormone.
Dalili nyingine ni kama
Matatizo kwenye uwezo wa kufanya tendo la ndoa mfano kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa,uume kushindwa kusima au kuwa mlegevu unaposimama.
Maumivu na uvimbe kwenye korodani
Kupungua au kutokuwa na ndevu na nywele za sehemu nyingine za mwili ,hii ni dalili ya uhaba au upungufu wa hormone ya testosterone.
VISABABISHI VYA TATIZO HILI
Kutengenezwa kwa mbegu inahusisha korodani na tezi iliyopo kwenye ubongo inayojulikana kama hypothalmus ambayo hii inahusika na kuzalisha hormone zinazochochea uzalishwaji wa mbegu za kiume. Matatizo katika viungo hivi huweza kupelekea tatizo hili.
Pia kuna weza kuwepo na matatizo katika maumbo ya mbegu za kiume nayo kupelekea tatizo hili.
Visabibishi vya tatizo hili ni kama ifatavyo:
SABABU ZA KIAFYA
1.Kuvimba kwa mishipa ya damu ya korodani-Varicocele ,hali hii inaathiri kiwango cha joto kwenye korodani hivyo kuathiri utengenezwaji wa mbegu za kiume.
2.Maambukizi, Baadhi ya maambukizi yanaweza kuathiri utengenezwaji wa mbegu za kiume na jinsi mbegu hizi zinavyotelewa nje.Magonjwa ya zinaa,magonjwa ya korordani yanaweza kupelekea kuziba kwa mirija ya manii na kuharibu seli zinazohusika na kutengeneza manii kwenye korodani.
3.Matatizo katika kutoa mbegu nje mfano tatizo la misuli ya shingo ya kibofu kutobana vizuri hivyo kupelekea shahawa kuingia kwenye kibofu cha mkojo badala ya kutolewa nje.
4.Kinga ya mwili kuziharibu mbegu.Kuna tatizo la kinga ya mwili kuzisoma mbegu za kiume kama wadudu wanaoleta magonjwa hivyo kuziharibu (sperm ant bodies)
5.Saratani, kuna baadhi ya saratani kama saratani ya tezi ya pituitari,saratani ya korodani zinaathiri pia utengenezwaji wa mbegu za kiume
6.USAWA WA HOMONI USIO SAWA (Hormone Imbalance):
Tatizo la homoni kutokuwa sawa si jambo linalowapata wanawake peke yao, ni jambo linalojitokeza pia kwa wanaume ingawa wengi wao huwa hawana muda wa kufikiri kuwa nalo. Homoni zina umhimu mkubwa katika kazi ya uzalishaji wa mbegu na katika afya ya uzazi wa mwanaume kwa ujumla.
Moja ya homoni kuu inayohusika na uzazi kwa mwanaume ni homoni ya testosterone. Kutokana na maisha yetu ya kisasa na baadhi ya matatizo yaliyoelezwa hapo juu upande wa uwingi wa mbegu, wanaume wengi wanajikuta katika hali hii ya kuwa na tatizo la homoni zao kutokuwa katika usawa unaohitajika kwa afya bora ya uzazi.
Vipo vitu vinavyoweza kuharibu homoni ya testerone na huanza kwa kuigiza au kijifanya vyenyewe ni estrogens (xenohormones). Estrogen ikizidi katika mwili wa mwanaume hupelekea uhanithi (uume kushindwa kusimama), kukosa hamu ya tendo la ndoa, kupungua kwa mbegu na kupungua kwa maji maji ya mbegu kwa ujumla.
Visababishi hasa vya kuharibika kwa testeroni ni pamoja na
• Vyakula vyenye soya
• Madawa yanayotumika katika mazao mashambani
• Homoni zinazoongezwa katika bidhaa za maziwa na nyama
• Vifaa au vyombo vya plastiki aina ya HDPE.
7.Mishipa ya manii kuziba
8.Madawa, Baadhi ya madawa mfano dawa za kutibu saratani,dawa za fangasi,na baadhi ya ant biotic zikitumika kwa muda mrefu zinaweza kusababisha tatizo hili.
9.Mfadhaiko (Stress) – Mfadhaiko au stress inaweza kuleta majanga makubwa katika homoni na kupelekea kushuka kwa uzalishaji wa mbegu za kiume.
Stress inahusika sana na tatizo la ugumba kwa wanaume wengi, na moja ya sababu ya stress hii ni ile hamu yenyewe ya kuwa na mtoto inapokujia kila mara kichwani.
Vile vile kuna presha kutoka kwa wazazi, ndugu jamaa na marafiki kwamba kwanini huzai. Hivi vyote ukiviweka kichwani na kuviwaza kila mara ni rahisi kwako kupatwa na tatizo la kupungua kwa mbegu na uzazi kwa ujumla.
Kuwa na amani, mwamini Mungu kwamba siku yako ipo, just relax kila kitu kina muda wake.
SABABU ZA KIMAZINGIRA
kemikali za viwandani kama benzene,toluene,xylene,dawa za kuua wadudu,rangi za nyumba, zinaweza kupelekea tatizo hili
Uvutaji wa Sigara – Uvutaji sigara, bangi na bidhaa nyingine za tumbaku huharibu ubora wa mbegu za kiume. Hilo halihitaji majadiliano. Habari njema ni kuwa madhara yaliyosababishwa na uvutaji sigara yanaweza kurekebishika ikiwa tu utaamua kuacha kuvuta. Huhitaji dawa kuacha kuvuta sigara, unahitaji kuamua tu kwamba sasa basi na hakuna lisilowezekana kwa mtu mwenye maamuzi na mwenye ndoto za maisha mazuri ya kiafya.
Vifaa vya kieletroniki – Tafiti zimeonyesha vifaa vingi vya kisasa vya kieletroniki vinasababisha kushuka kwa wingi na ubora wa mbegu kwa wanaume wengi miaka ya sasa kwani mionzi yake hupelekea joto lisilohitajika katika mifuko ya mbegu za kiume. Vifaa hivi ni pamoja na simu na Kompyuta.
Unashauriwa kutokuweka simu ndani ya mfuko wako wa suruali kwa kipindi kirefu na kutokuweka kompyuta mpakato (laptop) kwenye mapaja yako wakati wote ukiitumia. Ni mhimu pia kutokutumia masaa mengi kutwa nzima ukiwa kwenye kompyuta.
• Vifaa vya Intaneti visivyotumia waya – Siku hizi tofauti na zamani, kuna teknolojia mpya imeingia ya kuunganisha intaneti kwa kutumia vifaa visivyotumia waya (wireless internet) au kwa lugha nyepesi hujulikana kama Wi-Fi.
Vifaa hivi vinapunguza wingi wa mbegu, uwezo wa mbegu kukimbia na kuharibu muundo asili wa mbegu kwa ujumla (DNA fragmentation). Wanaume wenye tatizo la uzazi wanashauriwa kutotumia aina hii ya vifaa vya kuunganishia intaneti kwenye kompyuta zao na vile vile kutokuweka simu kwenye mifuko yao ya mbele ya suruali.
• Viuavijasumu na homoni katika vyakula – Viuavijasumu (pesticides) vinavyotumika katika mazao mbalimbali mashambani miaka ya sasa ni sababu mojawapo ya tatizo la homoni kutokuwa sawa kwa wanaume wengi.
Kwenye bidhaa nyingi za maziwa za viwandani sasa huongezwa homoni kama vile homoni ya estrogeni ambazo hazihitajiki katika mwili wako. Vyote hivi vina madhara katika afya ya mwanaume.
• Vyakula vyenye soya – Vyakula vyenye soya ndani yake hasa vile vya viwandani kama vile maziwa ya soya, burger za soya nk si vizuri kwa afya ya uzazi ya mwanaume. Vinasemwa moja kwa moja kuathiri ubora wa homoni ya testosterone homoni mhimu sana kwa afya ya uzazi wa mwanaume
.
• Unywaji pombe – Katika moja ya utafiti kwa wanaume wenye mbegu zenye ubora wa chini, matumizi ya kupitiliza ya unywaji pombe yalionyesha kuhusika na kupungua kwa mbegu za kawaida yaani mbegu nzuri zinazofaa kwa ajili ya uzazi.
• Matumizi ya vifaa vya plastiki – kuna baadhi ya vifaa vya plastiki vinapowekewa chakula cha moto hutoa kitu kijulikanacho kama ‘xenohormones’ ambacho huigiza kama ni ‘estrogen’ ndani ya mwili na hivyo kupelekea matatizo kwenye mfumo wa uzazi wa mwanaume.
• Joto kupita kiasi (Hyperthermia) – Mifuko ya mbegu za uzazi ya mwanaume inahitaji joto la chini kidogo ya lile joto la mwili kwa ujumla ili mbegu zibaki na afya. Inasemekana kuwa hii ndiyo moja ya sababu viungo vya uzazi vya mwanaume vipo karibu nje kabisa ya mwili wake.
Joto linajulikana wazi kuharibu ubora wa mbegu na hivyo itakuwa vizuri kuepuka mazingira ambayo yanaweza kusabbaisha joto la moja kwa moja kwenye viungo vya uzazi vya mwanaume ikiwemo kuepuka kuvaa nguo za ndani zinazobana sana.
• Mfadhaiko (Stress) – Mfadhaiko au stress inaweza kuleta majanga makubwa katika homoni na kupelekea kushuka kwa uzalishaji wa mbegu za kiume.
Stress inahusika sana na tatizo la ugumba kwa wanaume wengi, na moja ya sababu ya stress hii ni ile hamu yenyewe ya kuwa na mtoto inapokujia kila mara kichwani.
Vile vile kuna presha kutoka kwa wazazi, ndugu jamaa na marafiki kwamba kwanini huzai. Hivi vyote ukiviweka kichwani na kuviwaza kila mara ni rahisi kwako kupatwa na tatizo la kupungua kwa mbegu na uzazi kwa ujumla.
Kuwa na amani, mwamini Mungu kwamba siku yako ipo, just relax kila kitu kina muda wake.
• Aina ya chakula unachokula – Chanzo kingine cha kuwa na mbegu chache au zisizokuwa na afya ni kutokula chakula sahihi na cha kutosha kila siku. Kwa afya bora kabisa ya uzazi mwanaume anahitaji vyakula vyenye madini ya zinki (zinc) kwa wingi, selenium, Vitamin E, folic acids, Vitamini B12, Vitamini C na vyakula mbalimbali vinavyoondoa sumu mwilini (antioxidants).
Uzito kupita kiasi
JINSI YA KUJIKINGA
Njia kubwa ya kujikinga na tatizo la mbegu chache ni kula vyakula vyenye virutubisho vinavyosaidia kuongeza uzalishaji na ubora wa mbegu za kiume.
Njia nyingine ni pamoja na:
kuacha kuvuta sigara
kutokunywa pombe kupindukia
kutotumia dawa za kulevya
kuepuka msongo wa mawazo
kutovaa nguo zinazobana sana korodani
kupunguza uzito uliozidi
0 Comments