Ticker

6/recent/ticker-posts

Vyakula madhubuti kwa maendeleo ya ubongo wa mtoto


 




Miaka mitatu ya kwanza katika maisha ya mtoto ni muda ambao shughuli za ubongo wa mtoto zinahitajika kwenda kwa kasi kutokana  na ugeni alionao mtoto kuhusu mazingira na vitu vinavyo mzunguka. Je, unataka mtoto mwenye akili darasani?,  je, una wasiwasi na maendeleo ya ubongo wa mwanao. Hivyobasi, Karibu sana katika makala yetu hii hususani kipengele hiki cha Lishe na Mazoezi ambapo tunapata wasaa wakukufahamisha kuhusu masuala mbalimbali yanayo husiana na lishe pamoja na mazoezi.


Leo nakuletea elimu kuhusu vyakula ambavyo ni vya muhimu sana kwa mtoto anayeendelea kukua baada ya kuachishwa maziwa ya mama. Ifahamike kuwa, wakati wa utoto ndio kipindi pekee ambapo ubongo wa mtoto unaweza kutunzwa na hivyo kusaidia shughuli mbalimbali ambazo zitamuhitaji matumizi ya ubongo kama;


Kutunza kumbukumbu , Kutafsiri taarifa za mfumo wa fahamu , Kuelewa shuleni na kufaulu mitihani, n.k


Baadhi ya vyakula ambavyo vimefanyiwa uchunguzi na kuonekana vinasaidia katika maendeleo ya ubongo ni kama ifuatavyo;


Mayai,

Mboga za majani,

Samaki,

Maapple na matunda damu,

Mayai


Mayai ni mojawapo ya vyakula vyenye aina nyingi za virutubisho kama protini, wanga na mafuta ambavyo husaidia katika ukuaji na kuupa mwili  nguvu. Vivohivyo, mayai yanasaidia ukuaji wa ubongo wa mtoto kwakuwa yanatunza virutubisho vinavyoitwa choline na aside za mafuta yaitwayo omega-3 ambayo yanafanya kazi kubwa kipindi cha umri mdogo katika kuimarisha mpangilio wa muundo wa ubongo wa mtoto. 


Samaki


Samaki pia wanahitajika  kwa kiwango kikubwa kutokana na mchango wake katika kulinda ubongo ili usipunguze uwezo wake wa kufanya kazi na kuzuia upotevu wa kumbukumbu. Kazi hizi za ubongo husaidia watoto ambao wako katika miaka ya kwenda kusoma kuweza kuelewa na kukumbuka wanavyofundishwa darasani.


Maepple na matunda damu


Matunda haya yana kemikali iitwayo Quercetin ambayo hutumika kama dawa ya kuzuia athari za dawa nyingine zinazo haribu ubongo wa mtoto. Kemikali hii huweza ondoa sumu inayotokana na dawa hizi hivyo kusaidia ukuaji na ufanyaji kazi mzuri wa ubongo. Kemikali hii pia hupatikana katika mimea mingi kama mchaichai na mboga za majani kama sukumawiki.


Mboga za majani


Mboga za majani kama sukumawiki na spinachi, kwa kiwango kikubwa zinasaidia katika kulinda seli za ubongo na kusaidia ukuajia wenye afya.


Kwa namna moja ama nyingine wazazi wenye watoto wanatamani watoto wao wawe wenye akili na wanaojielewa na wenye kuyaelewa mazingira na vitu vinavyowazunguka kwa urahisi. Vyakula tajwa ni muhimu sana kwa mtoto ambaye amekwisha achishwa maziwa ya mama ili kumsaidia katika ukuaji ubongo na mwili kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments